Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa eo ameushukuru uongozi wa shirikisho la soka nchini TFF kwa kumteua kushika nafasi ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa kwa kusaidiana na kocha kutoka visiwani Zanzibar Hemed Morocco.
Mkwasa amesema wadhifa aliopewa na TFF, una hadhi kubwa kwake pamoja na kwa taifa zima la Tanzania, hivyo amewaomba mashabiki wa soka nchini kuwa na uvumilivu pamoja na kumuonyesha ushirikiano katika kazi yake hususan katika kipindi kigumu ambapo Taifa Stars inakabiliwa na mchezo wa mkondo wa pili wa kuwani kufuzu kucheza fainali za mataifa bingwa barani Afrika CHAN dhidi ya Uganda ambao wapo mbele kwa mabao matatu kwa sifuri.
Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.
Ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo June 24 alisema ‘Baada ya kutangaza kikosi cha wachezaji ambacho kitakuwa na kazi ya kubadili matokeo ya kufungwa mabao matatu kwa sifuri na kusaka ushindi wa zaidi ya mabao manne kwa sifuri ugenini huko jijini Kampala mnamo July 04′