Kamati ya utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Katika kikao chake cha leo
pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars)
ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama
sehemu ya tathmini ya mwenendo wa timu.
Kamati ya utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo:
1.Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia tarehe 21/June/2015.
2.Benchi lote la ufundi la Taifa stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.
3.Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)