Mwenyekiti wa Vijana CCM Mkoa wa Njombe Bwana Imani Fute Akitoa Taarifa
ya Wadhamini Zaidi ya Elfu Kumi Waliojitokeza Kumdhamini Lowasa Mkoani
Njombe
Lowasa akionesha majina ya wadhamini waliomdhamini Mkoani Njombe baada
ya kupokea toka kwa katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Cremence Mponji
Aliyesimama
Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike Akimkaribisha Edward
Lowasa Ili Awashukuru Wadhamini Wake na Wananchi Mkoani Njombe
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowasa Leo Amewasili Mkoani
Njombe Kuomba Wadhamini Katika Mchakato wa Kugombea Nafasi ya Urais
Mwezi Oktoba 25 Mwaka Huu.
Akizungumza
na Wanachama Waliojitokeza Kumdhamini Mbunge Huyo Pamoja na Wananchi
Mbalimbali Mjini Njombe Lowasa Amesema Endapo Watanzania Watamchagua
Kuongoza Taifa la Tanzania Hatokubali Kuendelea Kuona Watanzania
Wanaendelea Kuwa Masikini Ili Hali Taifa Lina Rasilimali za Kutosha.
Amesema
Endapo Atapata Ridhaa Hiyo Basi Ataendesha Nchi Kwa Mchakamchaka na Kwa
Atakayeona Anashindwa Kuendana Naye Basi Anatakiwa Kupisha Mapema Kwa
Lengo la Kuwakomboa Watanzania.
Suala la
Serikali Kununua Mahindi ya Wakulima Kwa Mkopo Amesema Hataki Kulisikia
Tena Endapo Atashinda Katika Uchaguzi Huo na Kwamba Kama Serikali
Itakopa Mazao Hayo Kwa Wakulima Basi Walipwa na Riba.
Imani
Fute ni Mwenyekiti wa Vijana CCM Mkoa wa Njombe Ambaye Amesema Katika
Mkoa wa Njombe Zaidi ya Wanachama Elfu Kumi Wamejitokeza Kumdhamini
Lowasa Katika Kinyang'anyiro Hicho.
Kwa
Mujibu wa Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe Bwana Clemence Mponji Amesema
Hadi Sasa Jumla ya Watia Nia 11 Katika Nafasi ya Urais Ndio Waliofika
Kuomba Wadhamini Katika Mkoa wa Njombe.