https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Wabunge 10 watikisa mjadala wa bajeti 2015



      Wabunge wakiwa wamesimama wakati spika wa bunge akiingia bungeni.Picha na Maktab

    Dodoma. Wakati Bunge likitarajiwa kupiga kura kesho kupitisha Bajeti, mjadala wa makadirio na matumizi hayo ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2015/16 ulitarajiwa na kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao, huku wabunge 10 wakitoa kauli ambazo zilisisimua chombo hicho cha kutunga sheria.
    Bajeti hiyo ya Sh22.49 trilioni iliyosomwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Juni 11, ni ya mwisho kwa Serikali ya Awamu ya Nne na iliangalia zaidi mafanikio na matatizo katika kipindi cha miaka mitano, hali iliyoweka mazingira mazuri kwa wabunge kugeuza mjadala kuwa wa kisiasa.
    Wakati wapinzani walitumia fursa hiyo kuonyesha kuwa Serikali haijafanya mambo makubwa na kuhitimisha kwa kuielezea kuwa “imechoka”, wabunge kutoka chama tawala walisifu kazi iliyokwishafanyika na kusifu awamu zote zilizotangulia kuwa zimeifanya Tanzania ing’are kiuchumi.
    Mjadala huo ndiyo uliozaa wabunge 10 ambao michango yao ilisisimua, kustua au kusababisha Spika au wasaidizi wake kuingilia kati kuweka mambo sawa.
    Mwandishi Wetu, Ibrahim Bakari, ambaye amekuwapo bungeni tangu bajeti hiyo iliposomwa, anachambua wabunge 10 waliotia fora na hata kuamsha hisia za upande mwingine au kutoa vionjo katika kuwasilisha michango yao.
    (1) Kangi Lugola (Mwibara CCM)
    Mbunge huyo machachari wa chama tawala aliibuka bungeni na staili ya aina yake wakati wa kujadili hotuba ya bajeti. Aliingia ndani ya ukumbi wa Bunge akiwa na begi lililojaa bidhaa za kawaida zilizoagizwa kutoka nje ambazo zinawezekana kutengenezwa nchini, akisema uagizaji huo ndiyo unaoporomosha thamani ya Shilingi ya Tanzania.
    Lugola, ambaye aliwahi kuingia bungeni na kofia ya kininja, ili afiche sura yake kwa watu aliotaka kuwasema waziwazi, alikuwa akiilaumu Serikali kwa kushindwa kuzuia bidhaa zinazotoka nje akisema fedha nyingi za kigeni zinatumika kwa matumizi ambayo hayastahili.
    “Nimekuja na kontena zima, kama ingewezekana kuingia nalo hapa, ningeingia nalo humu ndani,” alisema.
    Bidhaa alizoleta ni dodoki za plastiki kutoka China, soksi za Marekani, leso za China, chaki (Kenya), pipi (Kenya), nyembe (China), pamba za masikio kutoka China, vijiti vya kusafisha meno (China), bazoka (Kenya), viberiti (Kenya) pamoja na rula na penseli kutoka China.
    Alisema haiwezekani kwa Tanzania yenye rasilimali nyingi ambazo zingeweza kutumika kutengeneza bidhaa hizo, inatumia fedha za kigeni kuziagiza kutoka nje, “kisha tunalalamika kuporomoka kwa shilingi”.


    Alitoa pongezi za kejeli kwa CCM kuwa imeonyesha kioja cha aina yake kwa kuruhusu wagombea wengi wa urais “kama wametunga mshikaki” lakini akasema kiboko yao ni mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye anawania urais, atakapoingia madarakani.
    Sanya aliongeza kuwa “hiyo si demokrasia ni demo-crazy”.
    (3) Pauline Gekul (Viti Maalum, Chadema).
    Mbunge huyo ni miongoni mwa wabunge wa viti maalumu waliong’ara kwenye Bunge la Bajeti na kutoa sura mpya ya upinzani. Alitumia mjadala huo kuinanga CCM kiasi cha kuonekana kama ameishiwa pumzi.
    Huku akipigia chapuo upinzani kukamata dola, alisema: “Chadema wameishauri Serikali weee kwa kila kitu, lakini haisikii na hakuna kilichofanyika.
    “Hawa wenzetu tumefanya nao kazi sana kwa kipindi chote, tumefanya kazi kwa uaminifu, lakini CCM hawasikii… Nchi gani hii haisikii, nchi haina hata ndege, Yesu wangu! Kuendelea kuwashauri hawa watu, inahitaji moyo aisee.”
    Hata baada ya mwenyekiti wa kikao hicho, Lediana Mng’ong’o kumwambia kipindi cha kampeni bado, Gekul alisema: “Tulia mwenyekiti nipiwage sindano ipite vizuri, hawa watu hawasikii.”
    (4) Salum Barwani (Lindi Mjini, CUF)
    Kama wenzake wa upinzani alitumia muda mrefu kuinanga CCM. “Tutaipiga CCM kipigo kitakatifu, subirini hapo Oktoba 25 kwa kuwa imeshindwa kutekeleza ilani yake.
    “Ninaamini chini ya Profesa Ibrahim Lipumba, tutaipiga CCM kipigo cha aibu Lindi, tutaipiga kipigo kitakatifu mwaka huu. Profesa Lipumba ndiye mchumi wa kuiongoza Tanzania kupitia Ukawa …lakini akipitishwa na Ukawa,” alisema Barwani.
    Awali, Barwani alisema ana fomu kwa wanaotaka kuolewa na Profesa Lipumba kwamba zipo nafasi tatu, lakini mwenyekiti wa Bunge, Mng’ong’o alimkatiza na kumtaka afute kauli yake kwa kuwa ni udhalilishaji wa wanawake.
    Barwani alikubali kwa kusema: “Nafuta kauli mwenyekiti, lakini kama wewe hutaki, wapo wanaotaka mwenyekiti.” Baada ya kauli hiyo Bunge liliangua kicheko, naye akaendelea.
    (5) Suzan Kiwanga (Viti Maalum Chadema)
    Mbunge huyu ambaye Bunge hili ameibuka moto wa kuotea mbali, alianza kwa swali, Hivi mheshimiwa waziri unajua wafanyakazi wa Tazara wanadai Sh4.3 bilioni na unajua kama hawajalipwa mafao?
    Bila kusubiri jibu la waziri, aliendelea kutiririka akilalamikia tozo ya asilimia 10 ya mafuta ya taa, akisema yanatumika mijini na si vijijini ambako wananchi hawayawezi, kwa kuwa ni maskini sana.
    “Wabunge na mawaziri wanapewa magari V8 (Toyota Land Cruiser), huku ndiko fedha zinatakiwa zikatwe zipelekwe katika mfuko wa (mradi wa kusambaza umeme vijijini) REA. Haya tunatangaza utalii, utafanyaje utalii bila ndege, ukiulizwa (Waziri) utasema Ethiopia Airlines (Shirika la Ndege la Ethiopia), mmechoka tupeni nchi.”
    Kiwango alihitimisha kwa kutoa wito kwenye jimbo analotia nia akisema: “Kilombero nasema jiandikisheni kwa wingi, mambo yote ni Ukawa, jiandikisheni BVR.”
    (6) Ester Bulaya, Viti Maalumu, CCM.
    Bulaya, ambaye ni mbunge wa viti maalum (CCM), alianza kwa kupiga mkwara kuwa ameepuka kupooza, sasa yuko fiti na analitaka Jimbo la Bunda ambalo sasa linaongozwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira. Huku akizungumza kwa hisia, Bulaya alisema: “Hakuna sababu ya kuishabikia bajeti wakati baadhi ya mambo hayajakaa sawa, masuala ya vijana pamoja na tozo ambazo si sawa, lakini ilikoamuliwa kutozwa siko. Mafuta yanagusa maeneo mengi.
    “Eneo la kukata fedha ni safari za nje na ununuzi wa mashangingi, fedha nyingi zinatumika huku.”
    Bulaya, ambaye ni mwanahabari, alitaka Sheria ya Ununuzi ya Umma ifanyiwe marekebisho kwa kuwa ndicho kichaka cha wezi na wanapoiba anayekuja kubanwa ni Mtanzania wa kawaida.
    “Huku kwenye halmashauri nako, watu wanapiga sana hela. Mradi wa Sh2 bilioni zinaandikwa Sh10 bilioni, watu wanapiga sana huku.”
    (7) Magdalena Sakaya (Viti Maalum, CUF)
    Sakaya, ambaye ni naibu katibu mkuu wa CUF alirusha mashambulizi mfulizo ya hoja ambazo alizipanga vizuri. Alisema Serikali haisimamii mpango wake wa ununuzi wa magari na huku ndiko watu ‘wanapiga’ hela


    Katika hoja nyingine, Sakaya alilalamikia uuzaji holela wa fedha za kigeni, akitoa mfano maduka ya kubadilishia fedha yaliyoko Kariakoo na pia suala la uagizaji bidhaa za kawaida kutoka nje na uuzwaji wa bidhaa ghafi badala ya zilizoongezwa thamani.
    “Tunauza ngozi badala ya viatu, kwanini tusitengeneze viatu tukauza kwa bei nafuu,” alihoji.
    (8) David Kafulila, (Kigoma Kusini-NCCR-Mageuzi)
    Kafulila, ambaye alipata umaarufu kutokana na kuibua bungeni kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, alisema Serikali itapata laana kwa kushindwa kutekeleza sera ya wazee kwa miaka 10.
    “Mtapata laana, sera ikitungwa ni sheria, itekelezwe, mnawatapeli tu wazee wetu hawa,” alisema na kubainisha kuwa hakuna waziri wa kujibu hoja kwa kuwa wakati huo hawakuwapo bungeni kutokana na wengi wao kuwa kwenye harakati za urais.
    “Waziri wa fedha hawezi kujibu kila kitu, mmechoka,” alisema na kuishutumu Serikali kwa kutotoza kodi kwenye migodi.
    (9) Ezekiel Maige, (Msalala, CCM).
    Kwa sehemu kubwa ya hotuba yake alizungumzia ufisadi wa kutisha katika miradi ya maji na kilimo iliyoko Halmashauri ya Kahama.
    Akiichambua miradi hiyo alisema mradi wa maji katika Kijiji cha Bulige uliogharimu Sh700 milioni, umekwama kutokana na kukosa usimamizi wakati katika Kijiji cha Kagongwa walielezwa na wataalamu kuwa eneo hilo halina maji lakini waliwapuuza na wakatumia Sh430 milioni bila kupata maji.
    Ufisadi mwingine aliosema ni katika Kijiji cha Chela ambako kulikuwa na chemchem walioiendeleza kwa Sh500 milioni, lakini chemchem imezidiwa kwa kuwa mahitaji ya maji ni makubwa.
    Miradi ya kilimo iliyoko Kijiji cha Kahanga imegharimu Sh800 milioni lakini kwa uhalisia mradi unagharimu Sh130 milioni.
    (10) Anna Abdallah (Viti Maalum-CCM).

    Mwanasiasa huyo mkongwe alitumia muda mwingi kuwapongeza wanawake walio na nafasi kwenye uongozi wa kisiasa.
    “Nakupongeza mwenyekiti wa Bunge (Lediana Mng’ong’o) na Spika (Anne Makinda) ni mwanamke amefanya kazi nzuri. Ninawapongeza ACT kwa kuwa wana mwenyekiti mwanamke.
    “Nawapongeza NCCR-Mageuzi, makamu mwenyekiti ni mwanamke, ADC ambao katibu wao mkuu ni mwanamke, CUF ambao naibu katibu mkuu ni mwanamke, hii safi sana. Mimi siangalii chama, ninachoangalia ni nafasi ya mwanamke,” alisema mbunge huyo anayestaafu baada ya miaka 40 bungeni. Pamoja na wabunge hao , wengine ambao hotuba zao zilisisimua ni pamoja na Peter Msigwa (Iringa Mjini, Chadema), Moses Machali (Kasulu Mjini, NCCR-Mageuzi), Deogratias Ntukamazina (Ngara, CCM) na Cesilia Pareso ambaye ni mbunge wa viti maalumu wa Chadema.

    Credit: mwananchi
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Wabunge 10 watikisa mjadala wa bajeti 2015 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top