Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewashangaa makada wanaojinadi kuwa ni wasafi na waadilifu, akisema sifa hizo zinatakiwa zitolewe na jamii.
Jaji Warioba, mmoja wa watu ambao wamekuwa
wakikemea masuala ya ukiukwaji wa maadili, pia amesema hatamuunga mkono
mgombea ambaye anakiuka maadili ya uongozi.
Tayari makada 37 wamejitokeza kuomba ridhaa ya
wana-CCM kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wengi wao
wamekuwa wakijinadi kuwa ni wasafi na waadilifu na kuwataka wanachama
kutowapitisha watu wenye harufu ya ufisadi na wasio waadilifu.
Lakini Jaji Warioba alisema anaona wanakwenda kinyume na inavyotakiwa kufanyika.
“Viongozi wa sasa wanaonekana hawajali misingi ya
maadili kwa sababu jamii yetu yenyewe imeonyesha kutochukizwa na suala
hili la mmomonyoko wa maadili na wala jamii haijalipa uzito
unaostahili,” alisema Jaji Warioba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
Vuguvugu la uhuishaji wa Maadili kwa Jamii (Moral Rivival Movement).
“Viongozi wengi waliochukua fomu za kugombea urais
wanaonekana kujitangaza kuwa wao ni waadilifu. Jamii ndiyo ilipaswa
kusema kuwa viongozi hao ni waadilifu au sio waadilifu na sio wao
kujinadi,” alisema Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu.
Mkutano huo ulioandaliwa na viongozi wa dini kwa
kushirikiana na Chama cha Wataalamu wa Wakikristo (CPT) ulijadili ujenzi
mpya wa maadili katika jamii utasadia kupata kiongozi mwenye misingi ya
maadili ili kuepuka mitafaruku baina ya siasa za madaraka na siasa za
maslahi.
“Nimekuja hapa leo (jana) kuwaunga mkono katika
uzinduzi wa Vuguvugu la Uhaishaji Maadili kwa Jamii kwa sababu na mimi
ni sehemu ya mapambano hayo. Sitaunga mkono ng’o kiongozi yeyote ambaye
ataonekana kutokuwa na misingi ya maadili ya uongozi katika kipindi hiki
cha uchaguzi,” alisema Jaji Warioba.
Warioba, ambaye alieleza kuwa ameamua kukaa kimya
kuhofia kila anachosema kuhusishwa na masuala ya uchaguzi, alisema
viongozi ambao hawana maadili wamechangia kwa kiasi kikubwa kuwapo kwa
mianya ya rushwa.
“Lakini kama tunataka kuwa na viongozi wenye
misingi ya maadili, ni lazima tujenge upya maadili kwa sababu
tusipofanya hivyo yatazidi kuporomoka,” alisema waziri mkuu huyo wa
zamani.
Azungumzia suala la ubaguzi:
“Tumeona sasa ukabili umeanza kurudi, ubaguzi wa
kidini umeanza kurudi, ubaguzi wa kikanda umeanza kurudi, ubaguzi wa
namna hii umeanza kurudi kutokana na kukosekana kwa maadili,” alisema
Jaji Warioba ambaye alitumia muda mwingi kuishauri jamii kufuata misingi
ya maadili iliyoachwa na wasis
Profesa Beda Mutagahywa anena:
Akizungumzia maana ya Uhuishaji maadili( MRM),
Profesa Beda Mutagahywa alisema ni hamasa ya umma kwenda mbele kufikia
malengo fulani ya kijamii na malengo hayo yapo, yalikuwepo lakini hamasa
ya kuyafikia ilififia na hatimaye malengo yakasahaulika.
“Hii itasadia kama tutafanikiwa kuufanya uwe
ajenda na sehemu ya ilani ya vyama mbalimbali vya siasa katika uchaguzi
mkuu ujao,” alisema.
credit mwananchi