Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC, imesema haina mpango wa kurudia uandikishaji wapigakura katika maeneo waliyopita kwani inaamini kazi hiyo imefanywa kwa ufanisi wa hali ya juu.
Pamoja na hali hiyo NEC imewaonya wanasiasa kutoingilia kazi yao kwa sababu wanaifanya kwa mujibu wa sharia za nchi, na hawapo kwa ajili ya kumwonea mtu bali kuandikisha na kusimamia haki za wapigakura.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Waziri wan chi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Muhagama kusema kuwa NEC itafanya uchunguzi kubaini kama kuna ameneo ambayo wengi wameachwa bila kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura iliufanyike utaratibu wa kuandikisha.
Mwenyekiti wa NEC Damian Lubuva alisema hata kama hali hiyo itajitokeza, watarfikiria namna ya kurudia kazi hiyo, endapo utatolewa ushahidi wa wazi hasa kwa watu ambao hawakupata bahati.
“Siku ya mwisho kama kulikuwa na watu waliosalia ambao hawakuandikishwa kwenye vituo ambao hawakuandikishwa na waliorodheshwa na wanajulikana, tutafikiria, ikiwemo kurudia pale ambapo kutakuwa na ushahidi wa jambo hilo”Lubuva.
Alisema si wajibu wa NEC kwenda kutafuta watu eneo tofauti na lile lililopangwa kwa sababu hupangwa mapema mno baada ya kutolewa matangazo.
MTANZANIA
Wauguzi wa Zahanati ya Serikali katika kijiji cha Shishuyi Wilaya ya Maswa, wanadaiwa kumfukuza mjamzito Rotha Bujiku aliyefika katika Zahanati hiyo kwa ajili ya kujifungua na hatimaye kujifungua kwa taabu katika bafu la mkazi mmoja kijijini hapo karibu na Zahanati hiyo.
Watu walioshuhudia tukio hilo walisema lilitokea majira ya saa 2 asubuhi wakato Rotha alipofika katika Zahanati hiyo na kumkuta muuguzi Costansia John ambaye alikataa kumpokea.
Muuguzi huyo alikwisha kupewa maelekezo tangu awali kuwa anatakiwa ajifungulie katika hospitali ya Wilaya ya Maswa kwa kuwa amekuwa akizaa watoto mfululizo.
Wakati mama huyo akiendelea kulalamika kutokana na uchungu aliokuwa akiupata, muuguzi huyo alimpigia simu Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo na alipofika alimweleza mjamzito kuondoka eneo hilo.
Rotha alilazimika kuondoa katika eneo hilo kusogea jirani na Zahanati hiyo na kujifungulia bafuni.
MWANANCHI
Boniface Mkwasa anakuwa kocha ghali zaidi Mtanzania baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kumlipa Dola 12,500 (Sh28 milioni) kwa kukubali kuchukua jukumu la kuinoa Taifa Stars.
Hiyo ni baada ya TFF kuamua kumpa kocha huyo msaidizi wa Yanga, mahitaji yote pamoja na mshahara aliokuwa akipokea kocha Mart Nooij, aliyetimuliwa Jumapili iliyopita baada ya kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Uganda Cranes katika mchezo wa kusaka kufuzu kwa Chan 2016.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kuwa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo imekubaliana kwa pamoja kuwa Mkwasa apate stahiki sawa na zile za Nooij kama kielelezo cha kuonyesha jinsi ambavyo utawala wake unavyothamini makocha wazawa.
“Nilikutana na Mkwasa na kumwambia kuwa kile ambacho kocha aliyepita (Nooij) alikuwa anapewa, tutahakikisha naye anapata, kuanzia gari, posho nyumba na mshahara.
“Kwa kuwa suala la mshahara na nyumba ni jukumu la Serikali, tayari tumeshaiandikia barua kuwaambia kuwa tumeshapata kocha wa muda na tunaomba apate mahitaji yote ambayo aliyemtangulia aliyapata,” Malinzi.
Malinzi pia amewashukia wachezaji wa Taifa Stars pamoja na baadhi ya makocha kuwa wamechangia kwa namna moja au nyingine kufanya vibaya kwa Stars kwenye michuano mbalimbali inayoshiriki.
“Kama Shirikisho tunapambana katika mazingira haya magumu tuliyonayo kwani wachezaji wetu ni hawa hawa na hatuwezi kuchukua kutoka nje ya nchi.
“Sasa, watu wanamwangushia lawama Malinzi kama vile yeye ndiye anatakiwa kucheza wakati hiyo ni kazi yao wachezaji.
MWANANCHI
Mbunge wa Geita (CCM), Donald Max amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kuwa mbunge huyo alifariki jana saa 12.00 jioni katika hospitali hiyo.
Ndugai alisema Max alikuwa mahututi kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita.
“Taratibu za maandalizi ya mazishi kwa sasa bado maana ni kama dakika 15 zilizopita ndiyo kafariki,” Ndugai.
Max alizaliwa Mei 22 mwaka 1957 na kusoma katika Shule ya Msingi ya Salvatorian Convent na baadaye kujiunga na Shule ya Sekondari ya Azania mwaka 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1980 alikwenda nchini Urusi na kusoma kozi ya ufundi katika Chuo cha Ufundi chaRoston on Don kabla ya kujiunga na Taasisi ya Volgograd Polytechnical nchini humo na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika Uhandisi.
MWANANCHI
NIPASHE
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Harrison Mwakyembe amesema kufungiwa kwa Tanzania kuuza mcheze katika soko la Afrika Mashariki linashughulikiwa na litapitiwa ufumbuzi ndani ya miezi miwili.
Kauli ya Mwakyembe imekuja siku chache baada ya Baraza la mchele Tanzania RCT kuiomba Serikali kushughulikia kufunguliwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania wauze mchele katika soko la EA.
Mwakyembe alisema uamuzi wa kufungiwa kwa Tanzania naufahamu na jambo hilo linashughulikiwa.
Alisema hatua alizoanza kuchukua ni pamoja na kukutana na Waziri wa viwanda na biashara wa Rwanda kujadili suala hilo.
“Tatizo lilikuwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu waliokuwa wakiingiza mchele kutoka nje na kuuchanganya na mchele wa ndani kasha kasha kuuza katika soko la Afrika Mashariki,”Mwakyembe.
Alisema nchi wanachama wa EA wana sharia ya kusameheana ushuru wa bidhaa zinazozalishwa katika nchi hizo pamoja na kodi ndogondogo.
HABARILEO
Serikali imekubaliana na umoja wa madereva katika madai yao waliyokuwa wakihitaji yatekelezwe, hali ambayo imemaliza tishio la kuwepo mgomo kwa mabasi yanayoenda mikoani pamoja na yale yanayofanya safari mijini.
Madai hayo ni pamoja na kupewa mikataba ya kudumu na waajiri wao, kukatiwa bima za afya pamoja kuongezewa mishahara.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofikia makubaliano hayo, Katibu wa Umoja wa Madereva Nchini, Rashid Said alisema Serikali imekubali kusimamia na kutekeleza madai ya madereva ili kuepusha migomo ya mara kwa mara na kusababisha adha ya usafiri.
“Tumemaliza kikao chetu na mambo yote tuliyokuwa tunahitaji yatekelezwe yamekubalika. Lakini tumewaambia yatekelezwe ndani ya siku chache hizi na ifikapo Julai mosi mwaka huu kama hayajatekelezwa mgomo utakuwa pale pale,”Said.
Alisema wamefurahishwa na maamuzi ya kikao hicho ambayo yatakuwa ni mkombozi wa maisha ya madereva, kwani kwa muda mrefu wamekuwa hawanufaiki na kazi yao zaidi ya kuwazalishia wamiliki kiasi kikubwa cha utajiri, lakini wao kubaki katika hali duni ya maisha.
Hivi karibuni madereva walitishia kuanzisha mgomo endapo Serikali haitayashughulikia madai yao ambayo kwa muda mrefu wamekuwa wakipiga kelele yatekelezwe.
Mgomo wa madereva nchini ulitokea mwanzoni mwa Mei mwaka huu na kudumu kwa siku mbili na kusababisha kero mbalimbali kwa wasafiri huku asilimia kubwa ya wananchi wakitembea wakati wakienda katika shughuli zao mbalimbali huku waliokuwa wakienda mikoani kukwama katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo.
Hata hivyo, mgomo huo ulisitishwa baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda Tume ya kushughulikia madai ya madereva ambayo hadi jana ilikuwa ikiendelea kujadilian