Hivi ndivyo timu ya vijana ya Serbia ilivyopokelewa nchini kwao baada ya kutwaa kombe la dunia kwa kuifunga Brazil kwenye mchezo wa fainali
Mwishoni mwa juma lililopita, timu ya Taifa ya Serbia ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 imefanikiwa kutwaa kombe la dunia baada ya kuichapa Brazil kwa bao 2-1 katika mechi ya fainali na kufanikiwa kutwaa kombe hilo.
Mali wameshika nafasi ya tatu baada ya kuichakaza Senegal kwa goli 3-1 katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.