Rais wa FIFA Sepp Blatter ambaye alitangaza dhamira ya kwamba atajiuzulu June 2 2015 baada ya shirikisho hilo litakapompata Rais mpya.
Leo hii amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya mchekeshaji wa Uingereza Simon Brodkin kumfuata akiwa katika Press Conference alafu akamwagia pesa huku akijifanya kuwa yeye ni mjumbe wa FIFA kutoka Korea Kaskazini.
Simon Brodkin ambaye anafahamika kwa kupenda kufanya utani katika maeneo mbalimbali, amewahi kufanya utani kama huo 2014 baada ya kujiunga na timu ya taifa yaUingereza kama moja kati ya viongozi wa bodi na kutaka kusafiri na Kikosi cha Timu hiyo kilichokuwa kinasafiri kwenda Brazil kwenye Michuano ya Kombe la Dunia 2014.
Jamaa aliwahi pia kujiunga na kikosi cha Manchester City mwaka 2013 kama mchezaji wa timu hiyo na kufanya nao mazoezi kabla ya mechi yao na Everton kuanza.
Nimekusogezea video yatukio hili la leo jamaa alivyomwaga noti kwa Rais wa FIFA.
0 comments:
Post a Comment