https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    LAANA ZA EVA ZAITAFUNA CHELSEA

    carneiro vs mourinho
    Na Simon Chimbo
    Imeelezwa kuwa hali ya benchi la ufundi la Chelsea sio nzuri kwa maana ya umoja na maelewano yaliyokuwepo awali. Tangu Mourinho amfukuze katika benchi daktari mwanadada Eva Carneiro hakuna maelewano mazuri miongoni mwa staffs.
    Habari zinasema viongozi wote wa klabu hawajapenda kitendo cha kocha Jose Mourinho kumnyanyasa Eva ambaye alikua na mahusiano makubwa na viongozi pamoja na wachezaji.
    Kutokana na kilichotokea, kocha Jose Mourinho ambaye anashutumiwa kutumia maneno ya kibaguzi dhidi ya mwanadada huyo, amekua kimya kuomba msamaha hadharani wala kujutia maamuzi yake.
    Mastaa wa Chelsea pia wengi hawakupenda kilichotokea kwa daktari wao waliyemzoea na kuwa na mahusiano ya karibu na kila mmoja wao kikosini.
    Chelsea sasa imefungwa mechi tatu huku ikitoa sare mechi moja na kushinda moja. Rekodi mbaya tangu mara ya mwisho ilivyowatokea mwaka 1988.
    Wiki hii bado ni ngumu na ya mtego kwa Mourinho na Chelsea kwa ujumla. Wanacheza klabu bingwa Jumatano hii dhidi ya Maccabi Tel Aviv ugenini kabla ya kuja kupambana na Arsenal katika mchezo wa ligi kuu weekend ijayo.
    Wachezaji wanaonekana kutokuwa na njaa ya ushindi. Wamekata tamaa, wamechoka. Kuna maswali mengi nyuma ya pazia kuona kama wachezaji hawa huenda wamechoka mbinu na tabia za kocha wao. Ama kuna lolote kuhusiana na kutimuliwa kwa daktari wao?
    Mechi dhidi ya Arsenal inaweza kubadili kabisa upepo klabuni hapo. Chelsea na Mourinho wanahitaji matokeo ili angalau kuleta furaha klabuni. Kama wakifungwa na Arsenal, hakuna anayejua nini kipo kichwani mwa bosi Abramovich.
    Wataalamu wa mambo ya kandanda nchini England wanasema hakuna mchezaji hata mmoja anaecheza vizuri kikosini hapo. Wachezaji wote wanaonekana hawana ari ya kujituma wala ushindi.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LAANA ZA EVA ZAITAFUNA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top