Golikipa wa klabu ya Arsenal Peter Cech ambaye kwa sasa anatajwa kuwa ni golikipa bora Uingereza kwa mujibu wa takimu fupi za hivi karibuni kutoka katika mtandao wa metro.co.uk. Takwimu hizo ni kulingana na hatari alizookoa golini kwake katika mechi za Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015/2016.
Golikipa huyo wa zamani wa Chelsea amezungumza mtazamo wake kutokana na mwenendo wa klabu yake ya zamani ya Chelsea. Cech anaamini Chelsea wananafasi ya kuwania ubingwa msimu huu, licha ya kuwa wameanza vibaya msimu wa 2015/2016.
“Kiwango
chao kwa msimu huu kinanishangaza kwa sababu Chelsea ni moja kati ya
vilabu bora katika Ligi Kuu Uingereza. Hata hivyo sipo tena katika klabu
ya Chelsea hivyo ni ngumu kujua nini kinaendelea, ligi bado ndefu
lakini Chelsea bado ni timu nzuri machoni mwangu”>>> Peter Cech
Peter Cech ambaye msimu uliyopita alicheza katika klabu ya Chelsea na kufanikiwa kuisaidia timu hiyo kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza, alijiunga na Arsenal katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015 akitokea klabu ya Chelsea kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 11.
0 comments:
Post a Comment