Kauli hiyo imetolewa na mmoja wa wajumbe 32 wa kamati ya kampeni ya
CCM Dr Emmanuel Nchimbi ambaye kwanza anakanusha habari za kutaka
kukihama chama cha mapinduzi na kuongeza kuwa kuteuliwa kwa Dr Magufuli
na CCM kuwani urais si kwa bahati mbaya.
Mgombea urais wa chama hicho Dr John Pombe Magufuli akizungumza na
halaiki ya wakazi wa mji wa Moshi na viunga vyake ameendelea kusisitiza
kauli yake ya kuwataka watendaji wanaohusika na suala la ugavi wa umeme
Tanesco kuondoa tatizo la kukatika katika kwa nishati ya umeme ambalo
limekuwa kero kwa watanzania.
Pia Dr Magufuli amewaeleza watanzania namna ilivyo vigumu kujitolea
kupambana na ufisadi na kwamba kufanya kwake hivyo ni sadaka kwa
watanzania katika kuondoa mifumo kandamizi kwa baadhi ya viongozi wa
chama na serikali.
Dr Magufuli amefanya mikutano ya hadhara katika maeneo ya Usa river
mkoani Arusha, Siha, Hai na Moshi mjini ambapo ameungwa mkono na mamia
ya wananchi wa kada mbalimbali huku akifananishwa na sokoine huku
aliyekuwa katibu wa Chadema wilani Hai akikihama chama hicho na kujiunga
na CCM.
0 comments:
Post a Comment