……………………………………………….
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini
amewaasa wananchi kutosimama katika vituo vya kupiga kura mara baada ya
kupiga kura oktoba 25 mwaka huu kwani mawakala wa vyama vya siasa wa
kuwepo katika vituo vya kupigia kura ili kulinda maslahi ya chama pamoja
na wagombea wao.
Wito huo umetolewa na
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva alipokuwa
akifungua mkutano wa tume na waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi
wa uchaguzi na makamanda wa polisi nchini.
Jaji Lubuva amesema kuwa wajibu
wa mawakala ni kuangalia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume
zinazingatiwa katika mchakato mzima wa kupiga kura, kuhesabu kura na
kutangaza matokeo na pia kulinda maslahi ya chama au wagombea wao.
“Changamoto zilizojitokeza
katika chaguzi zilizopita ni pamoja na kuwapo na makundi ya vijana
wanaohisiwa kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kuwatisha wapiga kura
hasa wakinamama ili wasiende kupiga kura”
“Ni rai yangu kwenu kuhakikisha
hilo halijitokezi katika uchaguzi huu kwani kupiga kura ni haki ya
kikatiba ya kila mtanzania hivyo tusiruhusu vikundi vya watu kuwa
karibu na eneo la upigaji kura kwa kisingizio cha kulinda kura kwani
hii itapelekea uvunjifu wa amani” ameongeza Jaji Lubuva.
Mbali na hayo Jaji Lubuva
amesema lengo la kushirikisha Jeshi la polisi kwenye uchaguzi mkuu ni
kutambua na kuhakikisha kuwepo kwa hali ya usalama na amani wakati wa
uchaguzi kwani uchaguzi huru na wa haki ni lazima uendeshwe katika hali
ya utulivu na amani.
Kwa uapande wake Mkuu wa Jeshi
la Polisi nchini Ernest Mangu amesema kuwa jukumu la jeshi la polisi ni
kulinda usalama wa raia na mali zao, kuimarisha ulinzi katika vipindi
vyote na haswa kipindi hiki cha uchaguzi, kulinda vifaa vya uchaguzi na
kusimamia usalama katika vituo vya kupigia kura.
0 comments:
Post a Comment