Mchezaji Carlos Tevez amepata
mapokezi ya hisia kali yakichagizwa na ushindi wa jumapili wa Boca
Junior baada ya kuiongoza vyema kutwaa kwa mara ya 31 kombe la Ligi
ya Argentina.
Goli la kichwa kutoka kwa beki wa
kushoto wa Fabian Monzon lilitosha kuipatia ushindi mwembamba Boca
dhidi ya Tigre na kujihakikishia kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza
tangu 2011 huku wakiwa na mchezi uliobakia.
Kapteni Tevez, ambaye amerejea
kuichezea timu yake ya ujana ya Boca Julai mwaka huu, baada ya
kucheza ligi za nchi za nje kwa muongo mmoja, alijawa na furaha tele
baaada ya kupulizwa filimbi ya wisho.
Tevez akiwa na wachezaji wa Boca Junior wakifurahia kutwaa kombe
Carlos Tevez akijipinda kupiga mpira katika mchezo huo
0 comments:
Post a Comment