https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Ripoti ya CAG: Deni la Taifa lafikia trilioni 33.5, NEC yamulikwa, Mishahara hewa na Ukwepaji kodi..

    [​IMG]

    => Ulaji na uzembe vinatajwa kubeba sehemu kubwa ya ripoti hii.

    => Misamaha ya kodi 2014/15 ni asilimia 2 ya pato la taifa kinyume cha asilimia 1

    => Halmashauri 40 hivi ndo zenye hati safi kati ya halmashauri zaidi ya 160

    => Bidhaa a bilioni 9 za kupelekwa nje ziliuzwa hapa hapa nchini. Upigaji huo wa ukwepaji kodi.

    => Bidhaa za bilioni 89 za nje hakuna ushahidi kama zilienda Rwanda, Burundi na Uganda.


    => Rufaa za kodi nyingi mno zimedoda mahakamani na hivyo kuikosesha serikali kodi

    => Deni la Taifa hadi Juni 2015 lilifikia trilioni 33.5. Ndani ya mwaka mmoja lilikua kwa trilioni 7!

    => Malipo kwa deni kwa mwaka ni trilioni 4.

    => Deni na mishahara inamaliza mapato yote ya taifa. CAG anahoji, tutapata wapi pesa za maendeleo?

    => CAG Anataka maduka ya fedha za kigeni yadhibitiwe

    => Vyama vya siasa, kimoja tu kimewasilisha hesabu. Vyama 21 bado, Msajili afiatilie. Hajakitaja chama kilichowasilisha

    => Mishahara hewa katika Taasisi za umma 16 ni Shilingi bilioni 390. Mishahara ambayo haikulipwa na haikurejeshwa hazina ni bilioni 2


    => Sh. Milioni 700 za makato ya watumishi kwa Katavi na Kilimanjaro hayakuwasilishwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

    => Sh. Milioni 827 za vifaa vya upigaji kura zilitumika kwa kazi isiyo na tija katika Uchaguzi 2015


    => Nakala 158,003 za Katiba Pendekezwa hazikusambazwa kwa walengwa wakati wa mchakato wa Katiba Mpya

    => Manunuzi yenye thamani ya Sh. Bilioni 27 yalifanywa na Mashirika ya Umma bila ushindani


    => Cheti cha uendeshaji ATC kimeisha muda tangu 2010. ATC ina Wafanyakazi wengi kuliko kazi zilizopo

    => Bidhaa za bilioni 9 za kupelekwa nje ziliuzwa hapahapa nchini. Nia ni kukwepa kodi!

    => Bidhaa za Sh. Bilioni 89 za kwenda nje hakuna ushahidi kama zilienda Rwanda, Burundi na Uganda.


    => CAG ataka UDA irejeshwe serikalini. Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, Idd Simba aliwekewa sh. milioni 320 ktk akaunti yake binafsi.

    => Kampuni ya SAAFI inadaiwa Sh. bilioni 17. Hii ni ya mwanasiasa mkongwe, Mzindakaya.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ripoti ya CAG: Deni la Taifa lafikia trilioni 33.5, NEC yamulikwa, Mishahara hewa na Ukwepaji kodi.. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top