https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako atolea ufafanuzi sera ya Elimu Bure


    Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewataka walimu na maafisa elimu kusimamia vyema majukumu yao na kuhakikisha utoaji elimu bora kwa wanafunzi ili kupata wataalamu watakaolisaidia taifa.

    Waziri Ndalichako, ameyasema hayo Jijini Arusha, alipokutana na wakuu wa shule,maafisa elimu na watendaji wakuu wa idara za elimu ambapo amesisitiza nidhamu ili kusaidia matokea mazuri na ya haraka ya kuboresha elimu nchini.

    Waziri Ndalichako, amesema kuwa wataalamu mbalimbali ambao wanahitajia katika idara mbalimbali katika kukuza maendeleo wote wanahitaji zaidi mchango wa sekta ya elimu katika kuwapata wataalamu hao.

    Aidha katika ziara aliyoifanya katika mkoa huo wa Arusha, Waziri Ndalichako, ametoa ufafanuzi zaidi wa sera ya elimu bure ambapo amesema kuwa wazazi bado wanajukumu la kushirikiana na serikali katika kuwasadia watoto kupata elimu bora.

    Prof. Ndalichako amesema serikali haijawazuia wananchi wanaotaka kuchangia sekta ya elimu kutokana na changamoto zilizopo lakini haiko tayari kuona mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa sababu ya michango ya aina hiy
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako atolea ufafanuzi sera ya Elimu Bure Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top