Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mbunge wa viti maalumu(CHADEMA) Anastella Malack ambae amemaliza muda wake jana ametangaza rasmi kujiondoa CHADEMA na kurudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na chama cha ACT Wazelendo na kukabidhiwa kadi ya chama cha ACT Wazalendo
Malack alirudisha kadi hiyo hapo jana kwa kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazelendo Zitto Kabwe kwenye mkutano wa hadhara uluofanyika katika uwanja wa Kashaulili Mjini hapa
Katika mkutano pia aliyekuwa diwani wa Kata ya Makanyagio (CHADEMA) I ddy Nzyiguye alitangaza rasmi kujiunga na chama cha ACT baada ya kurudisha kadi ya CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya ACT wazelendo
Kabla ya kuwakabidhi kadi za Chama hicho Zitto Kabwe alipokea kadi za kutoka kwenye vyama mbalimbali ambazo wanachama wa vyama hivyo walimkabidhi na kasha aliwapatia kuwapatia kadi za ACT wazalendo
Katika hotuba yake ya kuwapokea walokuwa wanachama hao na viongozi kupitia chama hicho aliwataka viongozi wa ACT kutozitupa kadi hizo zilizo rudishwa wala kuzichoma moto na badala yake wazirudishe kwa makatibu wa Mikoa husika ambako wanachama hao waliko toka
Pia aliwataka wanchi wa Mkoa wa Katavi kuwachagua viongozi ambao wanania ya kuleta maendeleo kwa wananchi wao
Alisema wapo baadhi ya watu wnataka wachaguliwe kwa manufaa yao binafsi badala ya manufaa ya wananchi waliowachagua
Vilele aliwaambia Wananchi hao kuwa chama chake cha ACT wazalendo kitaweka wagombea wa nafasi za ubunge katika majimbo yote matano ya Mkoa wa Katavi na wagombea Udiwani katika kata zote 54 za Mkoa wa Katavi
Kwa upande wake aliyekuwa mbunge wa Viti Maalumu Annastela Malack aliwataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kushikamaene ili kuleta maendeleo katika Mkoa huo
Alisema Mikoa ya Katavi Tabora , Kigoma na Rukwa ipo nyumba kimaendeleo hivyo bila kuwepo na mshikamano ya wananchi wanao ishi kwenye mikoa hiyo maendeleo hayatakuwepo
0 comments:
Post a Comment