Utafiti uliofanywa nchini Swedeni
uliofanywa kwa watu milioni tano unaonekana kuunga mkono dhana kuwa
urefu wa mtu unauhusiano na kuugua ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo umebaini kuwa mtu
anavyozidi kuwa mrefu ndio anavyozidi kuwa katika hatari ya kuugua
saratani ya matiti, saratani ya ngozi pamoja na aina nyingine za
saratani.
Matokeo ya utafiti huo unapendekeza
kuwa kwa kila ongezeka kimo cha sentimita 10 juu ya urefu wa nchi 4,
baada ya mtu kukua kunahatari ya kusababisha saratani kwa asilimia 18
kwa wanawake na asilimia 11 ya wanaume.
0 comments:
Post a Comment