Bado tunahesabu saa kadhaa tu ili kuweza
kushuhudia michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji
wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika, michuano ambayo itaanza January 16, mwenyeji Rwanda kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Ivory Coast, baadae Gabon dhidi ya Morocco. Ninavyo vitu vinne ambavyo vinaweza kukuvutia kama utashuhudia michuano hiyo.
4- Rwanda ina wasichana warembo
Bara la Afrika mara nyingi huwa halikubaliki kwa vitu vingi ila Rwanda
kwa suala la kuwa na wasichana warembo kwa asilimia 100 wanatajwa kuwa
na wasichana warembo, hata kama ikitokea mmoja wao akakatisha barabarani
lazima ugeuze shingo.
3- Rwanda inatajwa kuwa
nchi ambayo imepambwa na maziwa vilima vidogo vidogo. Vilima ambavyo
kwa wageni watakaokwenda kuhudhuria michuano ya CHAN watapenda kuvutiwa navyo.
2- Ufunguzi wa michuano ya CHAN 2016 Rwanda
utafunguliwa au kuzinduliwa kwa ngoma za asili za nchi hiyo, kuna style
fulani hivi huwa wanacheza kama wanapaa, hii ni moja kati ya kivutio
cha mashabiki watakaopata nafasi ya kutazama michuano hiyo.
1- Baada ya kushuhudia mechi za michuano ya CHAN 2016, sio vibaya kama utatembelea Rwanda Volcano National Park (PNV), sehemu ambayo utapata nafasi ya kushuhudia sokwe wa milima hiyo ya Volcano.
0 comments:
Post a Comment