Timu ya Manchester United inaelekea kukamilisha mpango wa kumnunua kiungo kinda wa miaka 18 wa timu ya Benfica, Renato Sanches kwa kitita cha paundi milioni 46.
Rais wa Benfica Luis Filipe Vieira ameonekana Jijini London usiku wa Alhamisi katika kile kinachoaminika ni kukamilisha mpango huo.
Kwa sasa Sanches anamkataba na Benfica hadi mwaka 2021 na anauzwa kwa kitita cha paundi milioni 60, lakini anaweza kununuliwa kwa paundi milioni 31 kwanza na kisha baadaye kuongezewa paundi milioni 15.




0 comments:
Post a Comment